Burundi yapelekea kikosi chake cha kikanda nchini DRC
23 Agosti 2022Matangazo
Msemaji wa Jeshi la Burundi, Kanali Floribert Biyereke ameliambia shirika la habari la "The Associated Press" kwamba wanajeshi hao wapo nchini humo kwa jukumu rasmi.
Taarifa ya kuwasili kwa wanajeshi hao katika ardhi ya Kongo, pia imethibitishwa na msemaji wa jeshi la taifa Kongo huko Kivu Kusini, Luteni Marc Elongo, ambae amesema wanajukumu la kuyasaka, makundi ya ndani na nje ya taifa hilo yenye kujihami kwa silaha kwa lengo la kufanikisha amani.
Eneo hilo la lenye kupakana na mataifa ya Rwanda na Uganda, lenye hazina kubwa ya madini limekuwa na idadi kubwa ya makundi yenye kujihami kwa silaha.
Chanzo:afp