1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ndayishimiye abadili mawaziri wake

19 Novemba 2021

Baraza la mawaziri wa serikali ya Burundi limefanyiwa marekebisho, baada ya kufukuzwa kazi jana jioni waziri wa biashara, uchukuzi, viwanda na utalii kwa tuhuma za kuwa na mwenendo ulio kinyume na sera ya serikali.

https://p.dw.com/p/43Du1
Burundi Bujumbura | Evariste Ndayishimiye, Präsident
Picha: Bujumbura Amida Issa/DW

Mwingine aliofukuzwa kazi ni waziri wa sheria ambapo Rais Everiste Ndayishimiye amekuwa akikemea rushwa iliyokithiri miongoni mwa wanasheria nchini humo.  Mabadiliko hayo yametangazwa na Evelyne Butoyi ambea ni msemaji wa rais Evariste Ndayishimiye.

Katika marekebisho hayo mawaziri wawili ndio walioiaga serikali ikiwa ni pamoja na yule wa biashara, uchukuzi, viwanda na utalii Capitoline Niyonizigiye. Kifungu cha kwanza cha Sheria ya kirais iliyoo mfuta kazi kimesema waziri huyo amekuwa na mwenendo ulio kinyume na sera ya serikali.

Madai ya waziri kwenda Dubai na familia yake kwa fedha ya umma.

Weltausstellung Expo 2020 | Vereinigte Arabische Emirate | Dubai Exhibition Centre
Maonesha ya kibiashara ya kimataifa Expo 2020Picha: Ahmed Jadallah/REUTERS

Taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa wiki iliyopita waziri huyo alipoambatana na Rais Ndayishimiye kwenda Dubai kwenye maonesho ya kibiashara yaliyopewa jina ya Expo Dubai 2020 waziri Capitoline Niyonizigiye aliwaondowa kwenye msafara huo baadhi ya maafisa wa wizara yake na kuwawaeka watoto wake.

Pia waziri wa sheria Jenine Nibizi ameachishwa kazi. Rais Ndayishimiye amekuwa akiiosowa mara kwa mara wizara hiyo kukumbwa na rushwa na kwamba raia wamekuwa wakimfikishia malalamiko juu ya kesi kuchelewa na ziliokatiwa hukumu kutotekelezwa. Kwenye mkutano wa kuangazia taratibu za kufufuwa uchumi na kuifanya

Nia ya Rais Evariste NdayishimiyRipoti mpya yabainisha matukio ya mateso na mauwaji Burundie katika kukabiliana na rushwa.

Burundi kuwa nchi inayoinukia  rais Ndayishimiye Ripoti mpya yabainisha matukio ya mateso na mauwaji Burundialibaini kuwepo na maafisa serikali  ambao hawawajibiki na kwamba endepo hawatobadilika maendeleo ya nchi yataingia kwenye hatari. Katika marekebisho hayo aliye kuwa Waziri wa afya na kupambana na ukimwi Thaddee Ndikumana ambaye kakabidhiwa sasa wizara ya wafanyakazi wa umma ilokuwa ikiongozwa na Domine Banyankimbona ambaye kakabidhiwa wizara ya sheria.

Wapya katika serikali hiyo ni Sylvie Nzeyimana waziri wa afya na Leocadie Ndacayisaba waziri mpya wa habari na mawasiliano. Marekebisho hayo katika baraza la mawaziri wa serikali ni ya pili kufanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi 3 hivi tangu rais Evariste Ndayishimiye kuchaguliwa kuiongonza Burundi.

DW: Bujumbura