1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Burkina yaipongeza Mali kwa kulitaka jeshi la UN kuondoka

19 Juni 2023

Burkina Faso imeupongeza utawala wa kijeshi wa Mali kwa kile ilichosema ni "uamuzi wa kijasiri" baada ya Bamako kuutaka Umoja wa Mataifa kukiondoa kikosi chake cha kulinda amani cha MINUSMA

https://p.dw.com/p/4SkTF
Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop alitoa wito wa kuondolewa mara moja nchini humo kwa kikosi hicho cha kimataifa kilichoundwa mwaka 2013, na kuongeza kuwa ni uamuzi wa kimkakati wa serikali ya Mali katika mapambano dhidi ya ugaidi na kurejesha amani na usalama katika ukanda wa Sahel.

Soma pia: Mali yaitaka MINUSMA kuondoka nchini humo mara moja

Raia nchini Mali wanasubiri matokeo ya kura ya maoni juu ya katiba mpya iliyopigwa siku ya Jumapili ikiwa ni zoezi la kwanza la kidemokrasia kusimamiwa na utawala wa kijeshi.

Nchi za Mali na Burkina Faso zote zipo chini ya utawala wa kijeshi uliochukua madaraka kwa mapinduzi, na kwa muda mrefu zimekuwa zikipambana na uasi wa makundi yenye itikadi kali za kiislamu.

AFP