1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yawakamata Wafaransa wanne kwa ujasusi

20 Desemba 2023

Raia wanne wa Ufansa wamekamatwa nchini Burkina Faso kwa madai kuwa ni mawakala wa upelelezi duru za Burkina Faso na kidpomasia zimesem Jumanne.

https://p.dw.com/p/4aMmw
Burkina Faso | Ibrahim Traore
Kiongozi wa Burkina Faso, Ibrahim TraorePicha: AA/picture alliance

"Tunathibitisha kazi halisi ya wakazi hawa wanne wa Ufaransa wanaochukuliwa kuwa mawakala wa DGSE," kilisema chanzo cha Burkinabei, kikimaanisha huduma ya kijasusi ya kigeni ya Ufaransa.

Kulingana na jarida la Jeune Afrique, watu hao walikamatwa mapema mwezi wa Disemba katika mji mkuu wa Ouagadougou kwa tuhuma za ujasusi.

Kila liwezekanalo linafanyika ili kufanilisha kuwaachiliwa kwao," ilisema duru ya kidiplomasia ya Ufaransa. Nayo duru ya Burkina Faso iliongeza kuwa "Togo inasaidia kutafuta suluhisho."

Soma: Burkina Faso ni adui wa sera za Ufaransa, si watu wake

Uhusiano kati ya Burkina Faso na mkoloni wa zamani Ufaransa ulidorora baada ya jeshi kunyakua mamlaka katika mapinduzi ya 2022, kutokana na kushindwa kwa juhudi za kumaliza uasi wa kijihadi uliozuka mwaka 2015.

Viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, wakiongozwa na Kapteni Ibrahim Traore, baadaye waliamuru vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vikisaidia mapambano dhidi ya jihadi kuondoka nchini humo Februari mwaka huu.

Zaidi ya watu 17,000 wamekufa katika mashambulizi nchini Burkina Faso tangu mwaka wa 2015, kulingana na hesabu ya shirika lisilo la kiserikali liitwalo Armed Conflict Location and Event Data Project (ACLED). Watu milioni mbili wamepoteza makaazi yao kutokana na ghasia hizo.