1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yaishutumu France 24 'kuwasaidia magaidi'

28 Machi 2023

Baada ya kukifungia kituo cha televisheni cha Ufaransa, France 24, kufanya kazi zake nchini Burkina Faso, serikali ya nchi hiyo sasa inasema kituo hicho kilikuwa kikishirikiana na magaidi.

https://p.dw.com/p/4PMej
Frankreich | France 24 Zentrale
Picha: Alexander Klein/AFP/Getty Images

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso jana (Machi 27) ulitangaza kusitisha matangazo ya kituo cha televisheni cha France 24, baada ya kituo hicho cha Ufaransa kurusha hewani mahojiano kilichoyafanya na kiongozi wa kundi la Al-Qaeda tawi la Afrika Kaskazini.  

Msemaji wa utawala huo wa Burkina Faso, Jean Emmanuel Ouedraogo, amedai kwamba France 24 sio tu ni shirika la mawasiliano kwa ajili ya magaidi hao lakini pia linatoa uhalali wa vitendo vya magaidi na kauli za chuki.

Kituo hicho cha habari kilimuhoji kiongozi wa kundi la kigaidi la AQIM, Abu Ubayda  Yusuf al-Annabi.

Ouedraogo amesema wanaamini mahojiano hayo yaliyorushwa hewani ni sehemu ya mchakato wa kuhalalisha ujumbe wa magaidi na wanafahamu kuhusu athari za ujumbe huo nchini Mali.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW