1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Utawala wa kijeshi Burkina Faso wazuia mapinduzi

28 Septemba 2023

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umesema jana kwamba umezuia jaribio la mapinduzi siku ya Jumanne, ikiwa ni karibia mwaka mmoja tangu jeshi hilo lilipoingia mamlakani.

https://p.dw.com/p/4Wt8j
Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa burkina Faso Ibrahim Traore aliposhiriki moja ya sherehe za kitaifa mjini Ouagadougou. oktoba 15, 2022
Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa burkina Faso Ibrahim Traore aliposhiriki moja ya sherehe za kitaifa mjini Ouagadougou. oktoba 15, 2022Picha: Kilaye Bationo/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya jeshi iliyosomwa kupitia kituo cha televisheni cha taifa imesema idara za usalama na ujasusi za Burkina Fasozimefanikiwa kuzuia jaribio la mapinduzi lililopangwa kufanyika Septemba 26.

Kulingana na taarifa hiyo, maafisa na watu wengine wanaodaiwa kuhusika na jaribio hilo lililonuia kuvuruga utulivu wamekamatwa na wengine bado wanasakwa.

Kiongozi wa kijeshi nchini humo Ibrahim Traore aliingia mamlakani Septemba 30, 2022, baada ya mapinduzi ya pili yaliyofanyika katika kipindi cha miezi minane.

Mapinduzi hayo, kwa sehemu yalichochewa na kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa katika kukomesha uasi wa jihadi nchini humo.