1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Burkina Faso, Guinea na Mali wapanga ushirikiano

10 Februari 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa matatu ya Afrika Magharibi ambayo yanaongozwa kijeshi baada ya mapiduzi ya hivi karibuni wametaka ushirikiano wa kikanda

https://p.dw.com/p/4NKrC
Lage in Burkina Faso
Picha: Radiodiffusion Télévision du Burkina/AFP

Mawaziri hao ambao nchi zao zilipitia mapinduzi ya kijeshi wametaka ushirikiano katika biashara na kushughulikia tatizo la usalama.

Mawaziri hayo walikutana mjini Ouagadougou katika juma hili kwa lengo la kujadili ushirikiano.

Yote kwa pamoja yapo katika wakati mgumu wa kuwalinda raia dhidi ya ongezeko la makundi ya wenye kujihami na silaha, ambayo yamesababisha vikwazo vya kiuchumi na kuvuruga ushirikiano wa mataifa hayo wa kikanda na mataifa ya Magharibi.

Mataifa yote hayo matatu ya Afrika Magharibi yamekumbwa matukio ya mapinduzi tangu mwaka 2020, hatua ambayo imezorotesha jitihada za michakato ya maboresho ya kidemokrasia.