1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Bunge la Ukraine lakubali kujiuzulu kwa Kuleba

5 Septemba 2024

Bunge la Ukraine limekubali kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dmytro Kuleba.

https://p.dw.com/p/4kK8C
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ajiuzulu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ajiuzuluPicha: Virginia Mayo/File/AP/picture alliance

Wakati akihudumu kwenye wadhfa huo, waziri huyo hakuchoka kuziomba nchi za magharibi kuisaidia nchi yake baada ya kuvamiwa na Urusi.

Waziri huyo wakati wote aliomba msaada wa silaha za kuiwezesha Ukraine kujihami.

Hata hivyo kujiuzulu kwa Kuleba ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri kuwahi kufanyika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine miaka miwili na nusu iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa waziri wa mambo ya nje hakutaka kujiuzulu lakini amechukua hatua hiyo baada ya kushinikizwa na mkuu wa utumishi kwenye ofisi ya rais.