1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundestag yapitisha sheria kuhusu majaji wenye itikadi kali

23 Februari 2024

Bunge la Ujerumani limepitisha sheria itakayorahisisha mchakato wa kisheria kuwaondoa wale majaji wanaotizamwa kuwa ‘maadui wa katiba’.

https://p.dw.com/p/4cn0u
Ujerumani Berlin | Bundestag
Bunge la Ujerumani, Bundestag.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kwa kutumia sheria hiyo, mabunge ya majimbo au bunge la shirikisho yanaweza sasa kuiomba mahakama kuu ya katiba kumuhamisha jaji anayeshukiwa kutokuwa mtiifu kwa katiba.

Mnamo mwezi Agosti shauri liliwasilishwa dhidi ya mbunge mmoja wa chama chenye misimamo mikali cha AfD au chama mbadala kwa ujerumani  aliyekuwa pia  jaji.

Soma pia: Ujerumani yarefusha muda wa jeshi lake nchini Mali

Wizara ya Sheria ya Saxony ilimshtaki kwa kukiuka majukumu rasmi katika nafasi yake ya awali kama jaji katika Mahakama ya Dresden, mji mkuu wa jimbo la Saxony, mashariki mwa Ujerumani.

Awali maombi ya kumuondoa jaji, kumuhamisha au kumstaafisha yalipaswa kuwasilishwa chini ya miaka miwili baada ya tuhuma kutolewa.

Lakini sheria mpya imerefusha muda huo hadi miaka mitano.