1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani Bundestag limeunga mkono kwa wingi katiba ya Umoja wa Ulaya

12 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFE7

Bunge la Ujerumani,Bundestag limeidhinisha kwa wingi mkubwa katiba ya umoja wa Ulaya hii leo.Wabunge 569 wameiunga mkono katiba hiyo dhidi ya 23 waliopinga na wawili ambao hawakuelemea upande wowote.Kwa namna hiyo idadi ya waliounga mkono katiba ya umoja wa ulaya,imepindukia thuluthi mbili zilizokua zikihitajika.Kabla ya hapo kansela Gerhard Schröder aliwasihi wabunge waiunge mkono kwa wingi mkubwa katiba hiyo.Baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat litaipigia kura katiba hiyo may 27 ijao-siku mbili tuu kabla ya kura ya maoni ya katiba hiyo hiyo nchini Ufaransa.Wadadisi wanahisi kura ya ndio ya Ujeruma ni inaweza kushawishi matokeo ya kura ya maoni nchini Ufaransa.