1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ghana limepiga kura kufuta adhabu ya hukumu ya kifo

26 Julai 2023

Bunge la Ghana limepiga kura kufuta adhabu ya hukumu ya kifo. Ghana inakuwa nchi ya hivi karibuni kati ya mataifa 29 ya Afrika ambayo yamefuta hukumu ya kifo.

https://p.dw.com/p/4UOac
ECOWAS-  Nchi za Afrika Magharibi zimeweka vikwazo kwa Mali na Guinea
Rais wa Ghana Nana Akufo-AddoPicha: Nipah Dennis/AFP

Kulingana na ripoti ya kamati ya bunge, muswada huo mpya unalenga kurekebisha Sheria ya Makosa ya Jinai, ambapo nafasi ya adhabu ya kifo sasa itakuwa kifungo cha maisha jela. Ili ianze kutekelezwa, sheria hiyo lazima kwanza iidhinishwe na Rais Nana Akufo-Addo.

Hatua hiyo ni maendeleo makubwa kwa haki za binadamu

Mbunge Francis-Xavier Sosu, aliyewasilisha muswada huo ameielezea hatua hiyo kama maendeleo makubwa ya rekodi ya haki za binaadamu nchini Ghana. Idara ya Magereza nchini Ghana imesema hakuna mtu ambaye amenyongwa nchini humo tangu mwaka 1993. Hata hivyo, watu 176 walikuwa wamehukumiwa kifo hadi mwaka jana.