1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge Argentina kujadili muswada wa mabadiliko ya rais

1 Februari 2024

Bunge la Argentina limeanza kile kinachotarajiwa kuwa mjadala mrefu kuhusu muswada wa Rais Javier Milei wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kisiasa na hata masuala mengine ya maisha binafsi.

https://p.dw.com/p/4buQz
Buenos Aires, Argentina | Bunge likiwa katika vikao vyake.
Bunge la Argentina likiendelea na vikao vyake.Picha: Natacha Pisarenko/AP/picture alliance

Muswada wa Milei awali ulikuwa na vipengee 664 ila karibu nusu ya vipengee hivyo vimeondolewa katika majadiliano makali na upinzani ambao una idadi kubwa ya wabunge.

Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza nje ya bunge la nchi hiyo wakielezea kutoridhishwa kwao na muswada huo wa mabadiliko.

Soma pia:Waargentina wagoma, waandamana kumpinga Rais Milei

Wabunge wa upinzani wenye msimamo wa wastani wameonya kuwa wataufanyia mabadiliko zaidi muswada huo.

Kulingana na waandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP, polisi wamekabiliana na baadhi ya waandamanaji wakiwafyatulia mabomuya kutoa machozi.