1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga: Freiburg vinara wa ligi

5 Septemba 2022

Bayern Munich walikosa nafasi ya kurejea kileleni baada ya kudondosha pointi kwa wiki ya pili mfululizo. Nahodha wa Borussia Dortmund Marco Reus alifunga bao lake la pili msimu huu katika mechi dhidi ya Hoffeinheim.

https://p.dw.com/p/4GReP
GER, Bayer Leverkusen vs. SC Freiburg / 03.09.2022, BayArena , Leverkusen , GER, Bayer Leverkusen vs. SC Freiburg im Bi
Picha: Nordphoto/IMAGO

Bayern Munich walikosa nafasi ya kurejea kileleni baada ya kudondosha pointi kwa wiki ya pili mfululizo. Nahodha wa Borussia Dortmund Marco Reus alifunga bao lake la pili msimu huu katika mechi dhidi ya Hoffeinheim. 

Tuanzie na ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayern Munich wa waalikosa nafasi ya kurejea kileleni baada ya kulazimishiwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Union Berlin.  Huu ukiwa mfululizo wa kudodosha poiti kwa wiki ya pili mfululizo na kuwaweka mabingwa hao watetezi katika nafasi ya tatu kwenye jedwali wakiwa na poiti 11 nyuma ya Borussia Dortmund tofauti ya poiti moja.

Union Berlin haijashindwa katika mechi 12 za Bundesliga, tangu ilipofungwa 4-0 na Bayern mnamo Machi 2021.

Sheraldo Becker anaongoza kwa ufungaji wa mabao, akiwa na jumla ya mabao matano msimu huu. Hata hivyo Union haijawahi kuifunga Bayern katika majaribio saba wamesajili , sare tatu na kupoteza mara nne.

Mainz ilihitimisha kuanza kwa Bundesliga bila kushindwa kwa Borussia Moenchengladbach siku ya Jumapili huku beki wa kushoto Aaron Martin akifunga bao la pekee na la ushindi katika mtanange huo.

"Mbinu za kuudhi"

Kocha wa Bayern Julian Nagelsmann analaumu sare ya Bayern hio kutokana na kile alichokitaja kama mbinu za 'kuudhi' za wapinzani wao.

Fußball Bundesliga | TSG 1899 Hoffenheim - FC Bayern München | Nagelsmann
Julian Nagelsmann Picha: Weber/Eibner-Pressefoto/picture alliance

"Tulijua takwimu kabla ya mchezo na nadhani waliongeza idadi ya kututendea madhambi . Inaudhi sana kwa sababu unajaribu kumiliki mpira. unajaribu kupiga krosi na unapokuwa na dakika moja ya kugeuka na kupiga chenga mbele ya safu ya ulinzi ya mpinzani, lakini wanafachezea rafu ya kimbinu na inaudhi, lakini hiyo ni aina ya uchezaji na hiyo ni nzuri, kwa sababu sio rahisi kufanya hivyo na sirahisi kupata nafasi ya kufunga katika mbinu kama hii. "

Katika mechi nyengine Borussia monchenGladbach wangeweza kufikia pointi sawa na Bayern Munich wanaoshika nafasi ya tatu pointi sawa na Union Berlin kwa ushindi katika uwanja wa Borussia Park, lakini kadi nyekundu ya mchezaji  Ko Itakura katika dakika ya 53 iliaadhibu na dakika ya 55 wakapachikwa bao la pekee katika mechi hio iliyokamilika kwa moja bila.

Jana Jumapili, Hertha Berlin ilishinda kwa mara ya kwanza msimu huu na kufaulu kwa mabao 2-0 huko Augsburg huku Dodi Lukebakio na Marco Richter wakitikisa nyavu.

Freiburg wanaongoza jedwali la bundesliga kwa tofauti ya mabao kutoka kwa Borussia Dortmund,wakiwa na jumla ya poiti 12, sawa na Dortmund tofauti ya mabao.

Bao la pili msimu huu kwa Reus

Fußball Bundesliga | Borussia Dortmund vs Borussia Mönchengladbach
Picha: Moritz Müller/imago images

Nahodha Marco Reus alifunga bao lake la pili msimu huu. Ilikuwa ni mara ya 60 kwa Reus kufunga bao la kwanza katika mchezo wa ligi kuu. Dortmund sasa wamefunga angalau mara moja katika mechi 70 kati ya 71 zilizopita za ligi, isipokuwa 1-0 dhidi ya Borussia Mönchengladbach msimu uliopita.

Kocha wa Hoffeinheim Andre Breitenreiter amepoteza mechi tano za ugenini akiwa katika uga wa Signal Iduna Park dhidi ya Dortmund kama kocha.

Tuangazie sasa  Ligi ya Mabingwa, Paris Saint-Germain, kila msimu huanza na swali la kama huu unaweza kuwa mwaka wao wa ushindi ktika Ligi ya Mabingwa, ambayo itaanza kwa Kylian Mbappe na wachezaji wenzake dhidi ya Juventus kesho Jumanne.

Mchezo wa kwanza kabisa wa Frankfurt katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ni siku Jumatano nyumbani kwa Sporting Lisbon.

Borussia Dortmund watakuwa bila chipikizi Jamie Bynoe-Gittens watakapofungua kampeni ya kusaka ubingwa dhidi ya Copenhagen siku ya Jumanne na huku kukiwa na mashaka kwa kujumuishwa kwa Donyell Malen na Karim Adeyemi.

RB Leipzig wanatarajia kuweka nguvu zaidi baada ya mwanzo mbaya wa msimu wa Bundesligakatika mechi dhidi ya Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine.

Katika Tenis Novak Djokovic atakosa mechi za hatua ya makundi za Fainali ya Sebia Davis Cup inayotarajiwa kuanzia mjini Valencia wiki ijayo kutokana na sababu za kibinafsi.

Mchezaji huyo bora wa zamani wa dunia alishinda Wimbledon na kufikisha mataji yake ya Grand Slam hadi 21 lakini alikosa mashindano ya U.S. Open yanayoendelea baada ya kuamua kukataa chanjo ya COVID-19, jambo ambalo lilimaanisha kuwa hangeweza kusafiri hadi New York kwa ajili ya fainali ya mwaka huu.

 

AFP/ dpa