1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBulgaria

Bulgaria yanapiga kura uchaguzi wa tano katika miaka miwili

2 Aprili 2023

Wabulgaria wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa tano kuandaliwa katika miaka miwili, wakitumai kuuwekea kikomo msukomsuko wa kisiasa na kupambana na matatizo ya kiuchumi yanayochochewa na vita vinavyoendelea Ukraine

https://p.dw.com/p/4PbW4
Bulgarien Sofia | Parlamentswahl
Picha: Spasiyana Sergieva/REUTERS

Idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura inatarajiwa kuwa ndogo kutokana na kutojali kwa wapiga kura na kukatishwa tamaa na wanaisasa, ambao mara kwa mara wameshindwa kuiunda serikali ya muungano inayoweza kufanya kazi ipasavyo.

Zaidi ya hayo, katika siku za mwisho mwisho kabla ya uchaguzi huu, wimbi la vitisho vya mashambulizi ya bomu lilizilenga shule ambazo zinatumika kama vituo vya kupigia kura.

Watalaamu wa intaneti walisema vitisho hivyo vinatoka kwa makundi ya wadukuzi wa mitandaoni yanayohusishwa na Urusi na vililenga kuzusha hofu na kupunguza idadi ya wapiga kura.