1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:Waasi wakataa muda wa mwisho kusalimisha silaha

17 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0L
Kundi la waasi katika nchi ya Afrika ya Kati Burundi leo hii limekaata muda wa mwisho wa kusalimisha silaha zao katika kipindi cha miezi mitatu na kukomesha moja kwa moja vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimegharimu maelfu kwa maelfu ya maisha ya watu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Msemaji wa chama cha FNL mojawapo ya makundi madogo ya waasi linaloundwa kwa kiasi kikubwa na kabila la Wahutu lenye watu wengi nchini humo amesema kundi lake limekataa muda huo uliowekwa na viongozi wa Afrika baada ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani na kundi kuu la Wahutu hapo jana. Msemaji wa FNL Pasteur Habimana amesema hawawezi kuzungumza na Rais Domitien Ndayizeye kwa sababu yeye ni Mhutu na wao wanataka kuzungumza na Watutsi waliwauwa wao. Hapo jana Rais Ndayizeye ametia saini makubaliano ya amani na kiongozi wa kundi kuu la waasi la Kihutu Pierre Nkurunziza katika mkutano uliofanyika kwenye mji wa D'saalam nchini Tanzania ambao pia umehudhuriwa na viongozi wa eneo hilo.