1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:Pierre Nkurunziza ndiye rais mpya wa Burundi

19 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEje

Bunge la Burundi limepiga kura leo na kumchagua Pierre Nkurunzinza kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Hiyo ni hatua muhimu kuelekea amani kwa taifa hilo la Afrika ya kati lililojionea vita vya kienyeji kwa miaka 12 sasa.

Kiongozi huyo wa zamani wa waasi aliye wa kabila la Wahutu hivi sasa ndiye rais mpya baada ya kupata kura 151 kati ya kura 162.