1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA. Zoezi la kuwarudisha wakimbizi wa KIhutu laanza rasmi

14 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3e

Serikali ya Burundi imeanza rasmi leo zoezi la kuwarudisha kwa nguvu nchini Rwanda wakimbizi wa Kihutu ambao hapo awali walitoroka nchini Rwanda kwa hofu ya kufikishwa mbele ya mahakama za Gachacha.

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa wakimbizi hao wamo nchini humo kinyume cha sheria.

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Jean Marie Ngendahayo aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa hakuna tishio la usalama nchini Rwanda kwa hivyo wakimbizi hao hawana sababu ya kutoroka nchi yao.

Kamishna wa shirika la kutetea haki za wakimbizi la Umoja wa mataifa amesema Umoja wa Mataifa umeshtushwa na uamuzi uliochukuliwa na nchi hizi mbili na kuwa ikiwa Rwanda na Burundi hazitazingatia utaratibu maalumu wa kuwarudisha wakimbizi hao basi huenda zitavunja haki za kimataifa za wakimbizi.

Wakati huo huo mwandishi wetu kutoka Burundi ametuarifu kuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini humo bwana Paul Ngarambe, ameponea chupuchupu kuuwawa wakati alipokuwa njiani kuelekea magharibi mwa nchi hiyo.

Gari lake lilishambuliwa kwa risasi na watu wasio julikana. Burundi imo katika hatua ya kukamilisha utaratibu wa amani chini ya mkataba uliotiwa saini mjini Arusha, Tanzania na pande zinazohusika, hayo ni pamoja na uchaguzi wa kidemokrasi wa bunge utakao fanyika nwezi ujao