1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura: Ujumbe wa Umoja wa mataifa umeondoka Bujumbura jana ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFt5
baada ya ziara ya siku tano nchini Burundi.Lengo la ziara hiyo iliyowekwa siri ni kuzungumzia uwezekano kwa kikosi cha kulinda amani cha nchi za Afrika kuwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa.Ujumbe huo wa ngazi ya juu uliongozwa na naibu mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa la kusimamia opereshini za amani bibi Margaret Carey.Umoja wa Afrika umetuma nchini Burundi,tangu february iliyopita kikosi chake cha mwanzo cha kusimamia amani-wakiwemo wachunguzi 30 kusimamia makubaliano ya kuweka chini silaha na wanajeshi wapatao 2700 kutoka nchi za kiafrika.Ujumbe wa Umoja wa mataifa ulikua na mazungumzo pamoja na madhamana wa serikali ya mpito na wawakilishi wa umoja wa Afrika mjini Bujumbura.