1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura. Nkurunziza achaguliwa rais.

20 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjL

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Kihutu nchini Burundi Pierre Nkurunziza ameshinda kiti cha urais katika uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika Ijumaa katika kura ya bunge chini ya mpango wa amani wa kumaliza miaka 12 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeuwa watu zaidi ya 300,000.

Uchaguzi huo uliofanywa na mabaraza yote ya bunge la Burundi ambapo mgombea alikuwa mmoja tu, ilikuwa ni kilele cha chaguzi mbali mbali ambazo zimetoa madaraka kwa chama hicho cha zamani cha wapiganaji wa chini kwa chini cha Bwana Nkurunziza cha Forces for the Defence of Democracy FDD.

Demokrasia ya kudumu nchini Burundi inaonekana kuwa ni muhimu kwa ajili ya uthabiti wa eneo zima la maziwa makuu barani Afrika, eneo lililokumbwa na machafuko ya kikabila , mapigano ya kugombea mali pamoja na matatizo ya wakimbizi.