1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA: Machafuko yataka kuvuruga uchaguzi nchini Burundi

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7G

Milio ya risasi na miripuko imesikika katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura karibu na vituo vya kupigia kura.Maafisa wa usalama wamesema,mtu mmoja aliuawa na mwengine alijeruhiwa katika shambulio la gruneti.Katika shambulio jingine lililofanywa kwenye kituo cha kupigia kura,askari wa kulinda amani kutoka Afrika ya Kusini alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,machafuko hayo yadhihirika kuwa ni juhudi za kutaka kuvuruga uchaguzi wa mwanzo unaofanywa nchini humo tangu kuzuka vita kati ya waasi wa Kihutu na jeshi lililoongozwa na Watutsi.Inaaminiwa kuwa kiasi ya watu 300,000 waliuawa katika vita hivyo vilivyozuka mwaka 1993.