1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura: Chama cha FDD cha Burundi kimeshinda katika uchaguzi wa bunge

6 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEwt

Kikundi cha waasi wa zamani wa Kihutu katika Burundi kimeshinda uchaguzi wabunge katika nchi hiyo. Maafisa wanasema kwamba baada ya kuhesabiwa nyingi ya kura zilizopigwa, chama cha FDD kimepata baina ya asilimia 60 hadi 80 na kina uhakika wa kushinda. Chama hicho cha FDD kimesema kinataka kupambana na umaskini na kuendeleza mapatano na maridhiano baada ya Burundi kushuhudia miaka 12 ya uhasama wa kikabila baina ya jeshi la taifa linaloongozwa na Watutsi, kwa upande mmoja na waasi , kwa upande mwengine. Wabunge waliocvhaguliwa ndio watakaomchagua rais mpya hapo Agosti mwaka huu.