1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS ARIES : Fashisti wa Manazi atakiwa Chile

12 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFXm

Afisa mwandamizi wa serikali ya Chile amewasili Argentina kujadili kurudishwa nchini humo kwa fashisti wa zamani wa Manazi ambaye anatakiwa nchini Chile kwa madai ya kufanya mapenzi na watoto pamoja na kutesa watu.

Paul Schäfer mzaliwa wa Ujerumani alikamatwa katika mji mkuu wa Argentina hapo Ijumaa.

Serikali ya Argentina hivi sasa lazima iamuwe iwapo imrudishe Schäfer nchini Chile au inabidi isubiri maombi ya kumrudisha ambayo yumkini yakatoka Chile,Ujerumani na Ufaransa ambapo pia anatakiwa.

Schäfer mwenye umri wa mika 83 amekamatwa kwa madai ya kufanya mapenzi na watoto na tuhumu za kutesa wakati wa utawala wa dikteta wa zamani wa Chile Augusta Pinochet.Schäfer tayari amefunguliwa mashtaka na mahkama ya Chile kwa kuwadhulumu watoto kingono na anatakiwa nchini Ujerumani kwa madai hayo hayo.