1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES : Wafungwa 32 wamekufa gerezani kwa kuvuta moshi

17 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CER3

Wafungwa 32 katika gereza la Argentina wamekufa kutokana na kuvuta moshi uliosababishwa na moto uliowashwa na wafungwa waliokuwa wakipigana.

Wizara ya sheria ya Argentina imekanusha repoti za vyombo vya habari za awali kwamba wafungwa walikuwa wamefanya uasi wakitaka kuongezewa muda wa kutembelewa gerezani.Imesema tukio hilo limetokana na mapigano baina ya wafungwa wenyewe katika gereza hilo lilioko kwenye mji wa Magdalena.

Serikali imesema mapigano hayo yamezuka kwenye jengo la gereza lisilokuwa na ulinzi mkubwa ambapo wafungwa waliwasha moto kuzuwiya walinzi wasiingilie kati.