1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Buenos Aires. Bush ziarani Amerika kusini.

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEL2

Marais wa Brazil na Marekani wamekubaliana kufanyakazi kwa pamoja katika makubalino ya kibiashara ya dunia na kuepuka tofauti kati yao katika uhusiano wao wa kibiashara .

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema jana Jumapili kuwa mataifa hayo mawili yanaona kuwa ukamilishwaji wa mazungumzo ya shirika la biashara duniani WTO ya mjini Doha kuwa ni suala la kupewa umbele.

Rais wa Marekani George W. Bush ameongeza kuwa ni muhimu kufanyajitihada kuelekea kuundwa kwa eneo la biashara huria kutoka kaskazini hadi kusini mwa bara la Amerika .

Bush amewasili katika mji mkuu wa Brazil baada ya mkutano wa mataifa ya Amerika nchini Argentina , ambao umeshindwa kutatua tofauti juu ya kuundwa kwa eneo hilo la biashara huria .

Rais huyo wa Marekani , hivi sasa amewasili nchini Panama kwa mazungumzo zaidi na viongozi wa nchi hiyo. Ziara yake katika nchi za kusini na kati ya Amerika imegubikwa na maandamano yenye ghasia yanayofanywa na wale wanaopinga makubaliano ya kuwa na eneo la biashara huria pamoja na sera za Marekani duniani.