1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya

1 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEyN

Leo ndio ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair.

Bwana Blair anachukua mamlaka ya kuwa rais wa Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miezi sita .

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza bwana Jack Straw amesema ajenda Katika mkutano wa kumkabidhi mamlaka hayo bwana Blair, itakuwa juu ya suala la kuindihinisha katiba ya Umoja huo.

Mada nyingine inayotarajiwa kuchomoza kwenye mkutano huo ni suala la nafuu inayopata Uingereza kutokana na mchango wake kwenye bajeti ya Umoja huo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walishindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2007 hadi mwaka 2013 katika mkutano wa kilele mjini Brussels uliofanyika wiki mbili zilizopita.