1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Uturuki yakabiliwa na upinzani mkali wa Cyprus juu ya kujiunga na Umoja wa Ulaya

21 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZ8

Umoja wa Ulaya umeshindwa kukubali kutangaza juu ya kinyang'anyiro cha Uturuki kutaka kujiunga kwenye Umoja huo kufuatia upinzani uliojitokeza dakika za mwisho kutoka upande wa Cyprus.

Pendekezo lililotolewa liliitaka Uturuki kuikubali Cyprus kujiunga kwenye Umoja huo.Uturuki ambayo inashikilia nusu ya eneo la Kaskazini la kisiwa cha Cyprus imekataa kuitambua serikali ya Cyprus ya Kusini.

Wanadiplomasia wanasema Cyprus imekataa kuinga mkono Uturuki ili kusubiri kupitishwa mazungumzo ya mwisho juu ya suala hilo.

Mazungumzo juu ya Uturuki yamepangiwa kuanza mwezi ujao wa Oktoba.