1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels:Umoja wa Ulaya waisifu Rwanda:

9 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtj
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Umoja wa Ulaya wamesifu mafanikio ya kidemokrasia na kusameheana yaliyopatikana nchini Rwanda. Taarifa rasmi iliyotolewa na Baraza la Mawaziri imesema kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushiriki kwa dhati katika kuwachukulia hatua za kisheria wale waliohusika na mauaji ya halaiki mwaka 1994 nchini humo na utasaidia pia katika kuwanyang'anya silaha Wanamgambo wote. Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa Rwanda ina jukumu kubwa pia la kuwanyang'anya silaha Wanamgambo wote wa Kinyaruanda wanaopigana Kongo-Kinshasa na kuwarudisha tena katika maisha ya kawaida. Viongozi wa Rwanda wameombwa kutekeleza kwa dhati haki za Binaadamu na kusameheana. Miongoni mwa mambo muhimu ya kuangalia ni uhuru wa kusema na wa vyama vya kisiasa.