1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Tume ya Umoja wa Ulaya yapendekeza Uturuki kujiunga na Umoja huo

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEz0

Tume ya Umoja wa Ulaya kwa mara nyingine imependekeza Uturuki kujiunga na Umoja huo lakini sio kabla ya mwaka 2014.

Tume hiyo pia imesema hilo lifanyike iwapo tu Uturuki itafanya magaeuzi na kuutambua mgawanyiko wa Cyprus.

Katika mjadala wa muda mrefu mjini Brussels juu ya suala hilo,Makamishna walifikia uamuzi kwamba serikali ya Uturuki ipasishe sheria sita za mageuzi kabla ya kuanza kwa mazungumzo mwezi Oktoba ,tatu.

Uturuki iliutolea mwito Umoja wa Ulaya kutekeleza uamuzi ulioafikiwa na viongozi wake katika mkutano wake wa kilele mwezi Desemba iliyopita ambapo viongozi hao walikubaliana mazungumzo juu ya kujiunga kwa uturuki kwenye umoja huo yaanze mwezi Oktoba.