1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Suala la wakimbizi kuzingatiwa upya

13 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESW

Umoja wa Ulaya unadhamiria kuzingatia upya suala la wakimbizi kufuatia mmimniko wa wahamiaji wa Kiafrika katika maeneo ya Hispania ya Melilla na Ceuta kaskazini mwa Morocco.Umoja huo pia unataka kuimarisha misaada ya maendeleo kwa nchi za Kiafrika.Mjini Brussels,rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,José Manuel Barroso baada ya kukutana na Rais wa Umoja wa Afrika,Alpha Oumar Konaré,alisisitiza kwamba asili mia 40 ya Waafrika,kwa kila siku moja wana chini ya Euro moja kwa matumizi.Umasikini huo unapaswa kuondoshwa,ili kuweza kulitenzua tatizo la wakimbizi.Rais wa Umoja wa Afrika,Konaré ametuhumu vikali misaada inayotolewa na Umoja wa Ulaya kwa wakulima wake.Amesema ruzuku zinazotolewa kwa kilimo barani Ulaya ni sababu kubwa ya umasikini katika maeneo ya kilimo ya nchi za Kiafrika.Akaongezea kuwa tatizo la wakimbizi haliwezi kutenzuliwa kwa kuwatia watu jela na kujenga kuta.