1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels:Sheria mpya ya China yakosolewa na Umoja wa ulaya

15 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWz

Umoja wa Ulaya umesema umeingiwa na wasi wasi kutokana na sheria mpya ya jamhuri ya umma wa China inayotishia kuzusha vita ili kuizuwia Taiwan isijitangazie uhuru.Umoja wa Ulaya umezitolea mwito pande zote mbili zijizuwie na aina yoyote ya uamuzi wa upande mmoja na kusaka ufumbuzi kwa njia ya majadiliano.Marekani nayo pia imeikosoa sheria hiyo.Msemaji wa ikulu ya marekani amesema sheria hiyo mpya haitosaidia kuleta amani na utulifu katika eneo hilo.Sheria hiyo mpya inairuhusu jamhuri ya umma wa China kutumia nguvu za kijeshi ikilazimika,kuzuwia Taiwan isijitangazie uhuru wake.Walinzi wa mazingira-Die Grüne nchini Ujerumani,wametoa mwito vikwazo vya silaha vya umoja wa ulaya dhidi ya China viendelezwe.Kansela gerhard Schröder lakini amekua akipigania vikwazo hivyo viondolewe.