1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels:Maafisa wa kibalozi wa EU washindwa kuafikiana juu ya Uturuki.

29 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWT

Wanabalozi wa nchi za Umoja wa ulaya-EU, wameshindwa tena kukubaliana juu ya mfumo wa mazungumzo yanayotarajiwa kuanza na Uturuki wiki ijayo. Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi 25 wanachama watakua na mkutano wa dharura mjini Luxembourg Jumapili ijayo. Maafisa wa kibalozi wamesema kwamba Austria imekata kuacha msimamo wake kwamba , lazima Uturuki ipewe tu nafasi ya kuwa mshirika na sio uwanachama kamili. Mazungumzo rasmi juu ya jaribio la Uturuki kutaka uwanachama katika Umoja wa Ulaya, yanatazamiwa kuanza Jumatatu ijayo.