1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wajumbe wa Umoja wa Ulaya waahirisha mazungumzo.

17 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWO

Wajumbe wa Umoja wa ulaya hatimae wameamua kuya ahirisha mazungumzo yaliopangwa kuanza leo baada ya Croatia kugoma kutimiza agizo la kumtoa mtuhumiwa mkuu wa uhalifu wa kivita Generali Ante Gotovina kwa mahakama ya uhalifu ya umoja wa matifa huko The Hague.

Gotovina anatuhumiwa kuamrisha mauaji ya waserbia 150 na kuwafanya waserbia wengine 150,000 kuyatoroka makaazi yao wakati Croatia ilipo teka jimbo la Krajina katika vita vya mwaka 1995.

Huko Zaghreb Generali Ante Giotovina anachukuliwa kama shujaa na Wacroatia wengi.

Uamuzi huo wa wajumbe wa Umoja wa Ulaya ni ishara kwa nchi zinazo tarajia kupata uanachama wa umoja wa Ulaya kuwa ni lazima kutimiza masharti yanayo takikana na umoja huo.