1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Waafrika wanaoingia katika umoja wa Ulaya, mawaziri kulijadili suala hilo.

12 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESl

Mawaziri wa sheria wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo Jumatano kuangalia njia za kushughulikia suala la kuongezeka hivi karibuni kwa wahamiaji wa Kiafrika wanaojaribu kuingia katika mataifa ya umoja huo kupitia katika maeneo yanayomilikiwa na Hispania , kaskazini ya pwani ya Morocco. Waafrika 11 wameuwawa katika wiki za hivi karibuni wakati wakijaribu kuruka uzio katika mpaka wa Melilla na Ceuta.

Baadaye , mawaziri hao watajadili suala la hilo la kamishna wa umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya wakimbizi Antonio Gutteres.

Hii inakuja siku moja baada ya Morocco kuwarejesha mamia ya watu hao nchini Senegal.

Siku ya Jumatatu watu 280 walirejeshwa nchini Senegal.