1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakutana mjini Brussels

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF33

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussles kujaribu kuiokoa katiba mpya ya umoja huo na kumaliza mzozo wa bajeti. Uingereza inasema haitakubali kukiachilia kiwango cha euro milioni tano inachokipokea kutoka kwa umoja wa Ulaya kila mwaka.

Waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker, ambaye atakuwa mwenyekiti katika mkutano huo wa siku mbili, amesema ana wasiwasi ikiwa makubaliano kuhusu bajeti ya mwaka 2007 hadi 2013 yataafikiwa.

Rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso, amesema ikiwa kikao hicho kitashindwa kuutanzua mzozo wa bajeti na kutafuta njia za kuiokoa katiba, umoja wa Ulaya utatumbukia katika mzozo wa kisiasa. Katiba ambayo ni lazima iidhinishwe za mataifa yote 25 wanachama, ilikatiliwa na wafaransa na wadachi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, alisema hatakamilisha kuidhinishwa kwa katiba hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho na mahakama.