1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Viongozi wa umoja wa Ulaya wajadili ugaidi wa kimataifa mjini Brussels

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtF

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujadili njia zitazotumiwa kukabiliana na ugaidi wa kimataifa. Hatua ambazo tayari zimepitishwa na mawaziri wa mambo ya ndani na wa sheria wa mataifa hayo zinatarajiwa kuidhinishwa katika kikao hicho.

Mada nyengine zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran, hali ya mashariki ya kati na mazungumzo ya Uturuki kutaka kujiunga na umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa hivi karibuni, asilimia 35 ya wanachama wa umoja wa Ulaya wanauunga mkono mpango wa kuiruhusu Uturuki iwe mwanachama wa umoja huo. Kura hiyo pia imedhihirisha kuungwa mkono kwa idadi ndogo ya kura, kwa Romania na Bulgaria ambazo zinasuburi kuwa wanachama mwaka wa 2007.