1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya yataka China iondolewe vikwazo vya silaha

19 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVe

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya anataka kuwekewa vikwazo vya silaha kwa China kuondolewe ifikapo mwezi wa Juni.

Jean Asselborn ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Luxembourg kufuatia mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa China Li Zhaoxing ameahidi kuushinikiza Umoja wa Ulaya kukomesha uwekaji wake wa vikwazo vya silaha dhidi ya China.

Hata hivyo sheria ya China iliopitishwa hivi karibuni ya kupinga harakati za kutaka kujitenga kwa Taiwan ambayo inaweza kuruhusu matumizi ya nguvu dhidi ya kisiwa hicho imetishia kuvuruga mipango hiyo.

Umoja wa Ulaya uliiwekea China vikwazo vya silaha kufuatia mauaji katika Uwanja wa Tianmen hapo mwaka 1989.