1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wataka utulivu Kongo

3 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPK

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imetoa mwito kuwe na utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku kura zikiendelea kuhesabiwa nchini humo.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa yana wasiwasi machafuko huenda yakazuka kufuatia machafuko yaliyotokea wakati wa kampeni na hatua ya vyombo vya habari kutafsiri matokeo ya awali kimakosa.

Baadhi ya runinga za kibinafsi zinazomilikiwa na wagombea zilionyesha matokeo katika miji na vijiji, zikiyaonyesha kama mkondo wa kitaifa katika matokeo ya uchaguzi wa Kongo. Matokeo ya mwisho hayatarajiwi kutangazwa kabla Agosti 30.