1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wafikiria kuweka jeshi la kulinda amani Lebanon.

17 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6n

Wakati huo huo umoja wa Ulaya unafikiria kuweka jeshi la kulinda amani nchini Lebanon katika juhudi za kujaribu kusitisha mapigano kati ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Finland Erkki Tuomoija, ambaye nchi yake inashikilia hivi sasa urais wa umoja wa Ulaya , amesema kuwa inawezekana kuwa umoja wa Ulaya ama umoja wa mataifa ukawa na jukumu la kulinda amani katika eneo hilo.

Hakutoa maelezo zaidi, lakini amesema , jeshi lolote linaonekana kuwa ndio suluhisho la muda mrefu katika mzozo huo wa Waisrael na Waarabu.

Tuomoija ambaye alikuwa mjini Brussels kwa ajili ya mkutano wa mawaziri 25 wa umoja wa Ulaya , amesema mawaziri hao wanapanga kutoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja na kuachiliwa kwa wanajeshi wawili wa Israel waliokamatwa na wapiganaji wa Hizbollah wiki iliyopita.