1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wachunguza ombi la Iran kutaka mazungumzo juu ya mpango wake wa nyuklia yaanze tena

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKi

Umoja wa Ulaya unalichunguza pendekezo la Iran kutaka mazunguzo juu ya mpango wake wa nyuklia yaanze tena. Hakuna uamuzi uliotolewa juu ya barua iliyotumwa kwa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani na mpatinishi mkuu wa Iran katika mzozo huo wa nyuklia.

Mataifa hayo matatu, wanachama wa umoja wa Ulaya, yamekuwa yakiongoza mazungumzo na serikali ya Tehran juu ya mpango wake wa nyuklia huku Marekani ikiilaumu Iran kwa kutengeneza silaha za kinyuklia. Lakini Iran kwa upande inashikilia kwamba inataka kutumia teknolojia ya nyuklia kwa amani. Umoja wa Ulaya unataka Iran isitishe shughuli zake zote za kurutubisha madini ya uranium.