1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Umoja wa Ulaya waapa kupambana na ugaidi wa kimataifa

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEue

Kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyofanywa na magaidi mjini London, umoja wa Ulaya umeapa kuongeza juhudi zake za kupambana na ugaidi wa kimataifa. Mawaziri wa sheria na mambo ya ndani wa umoja huo walikubaliana katika mkutano wao mjini Brussels juu ya hatua za usalama zinazotakiwa kuanza kutekelezwa mara moja. Hii ni pamoja na kuhifadhi ushahidi wa simu zinazopigwa na matumizi ya mtandao wa mawasiliano wa internet.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Uingerezal bwana Tony Blair ametoa mwito kuanzishwe sheria kali zitakazotumiwa kuwaruhusu watu kuingia Ulaya na watu wanaotuhumiwa kuhubiri uhasama na itikadi kali ya kiislamu wasiruhusiwe kuvuka mipaka ya mataifa ya umoja wa Ulaya. Blair pia amesema atafanya mkutano na viongozi wa kiislamu nchini Uingereza katika juhudi za kuendeleza uislamu wa kweli.