1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya upo tayari kuchangia vikosi vya amani

2 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPk

Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa Israel na wanamgambo wa Hezbollah wasitishe mapigano moja kwa moja.Taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Brussels na mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi 25 katika Umoja huo,baada ya kuwa na mabishano makali,imesema nchi hizo zipo tayari kuchangia vikosi katika tume ya kimataifa kulinda amani nchini Lebanon.Umoja huo vile vile kwa hivi sasa,umepinga kuliweka kundi la Hezbollah katika orodha ya mashirika ya kigaidi.Chama cha Wapalestina cha Hamas,ni miongoni mwa makundi yaliokuwemo katika orodha hiyo ya magaidi.