1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels: Umoja wa ulaya, unafikiria uwezekano wa kutathimini upya ...

3 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvb
vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya jamhuri ya umma wa China.Hayo ni kwa mujibu wa kamishna anaeshughulikia masuala ya biashara Pascal Lamy.Duru za kidiplomasia zinasema msimamo huo wa bwana Pascal Lamy unaambatana na misimamo ya mwenyekiti wa kamsheni kuu ya Umoja wa Ulaya Romano Prodi na kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder.Akiwa ziarani nchini China,kansela Gerhard Schröder ametetea haja ya kuondolewa vikwazo vya silaha dhidi ya nchi hiyo.Msimamo huo wa kansela unakosolewa lakini nchini Ujerumani.Mwenyekiti wa kamati ya haki za binadam ya bunge la shirikisho Bundestag,mbunge wa chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne,Christa Nickel ameliambia gazeti la "Die Welt" haiungi mkono fikra hiyo."Lawama zimesikika pia toka upande wa upinzani wa CDU na FDP.Umoja wa Ulaya uliiwekea China vikwazo vya silaha baada ya vikosi vya usalama kuyakandamiza maandamano ya wanafunzi katika uwanja wa amani Tianan men katika mwaka 1989.