1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya kufufuwa mpango wa uchumi

20 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVF

Umoja wa Ulaya wiki hii utajaribu kufufuwa mipango ya kijasiri ya kuboresha uchumi unazorota wa bara hilo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana hapo Jumanne na Jumatano kwa ajili ya mkutano wao wa jadi wa kipindi cha majira ya chipukizi ambao mwaka huu unakuja wakati mpango unaojulikana kama Agenda ya Lisbon uliozinduliwa mwaka 2000 kwa lengo la kuufanya uchumi wa Ulaya kuwa mojawapo ya uchumi wenye kutowa ushindani mkubwa nusu yake ukiwa umekamilika.

Kuzorota kwa muda mrefu kwa uchumi wa bara hilo karibu kumeufanya mpango huo utelekezwe kabisa wakati mataifa makuu ya Umoja wa Ulaya Ujerumani na Ufaransa yakiendelea kupambana na hali ya ukosefu wa ajira ambayo ni zaidi ya asilimia 20 katika nchi zao.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Ujerumani kimefikia rekodi mpya ya juu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha baada ya vita cha asilimia 12.6.