1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya kuanza mazungumzo na Bosnia-Herzegovina

20 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQ8

Kamishna wa Ulaya anayeshughulikia kupanuliwa kwa jumuiya ya Ulaya, Oli Rehn, amependekeza mazungumzo yaanze kati ya jumuiya hiyo na Bosnia-Herzegovina, inayotaka kujiunga na umoja huo.

Ameyasema haya siku moja baada ya bunge nchini Bosnia kuidhinisha mpango wa kulifanyia marekebisho jeshi la polisi lililogawanyika kwa misingi ya kikabila. Hata hivyo umoja wa Ulaya utachunguza ikiwa Bosnia itautekeleza mpango huo. Tarehe ya kuanza kwa mazungumzo hayo bado haijatangwazwa.