1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Solana ataka vikwazo vya silaha dhidi ya China viondolewe

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFU9

.

Mkuu wa masuala ya sera katika jumuiya ya Ulaya Bwana Javier Solana amesema kuwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya China ni si haki. Jumuiya ya Ulaya iliweka vikwazo vya mauzo ya silaha dhidi ya taifa hilo la kikomunist kufuatia mauaji ya mwaka 1989 katika uwanja wa Tiananmen mjini Beijing.

Bwana Solana amewaambia waandishi wa habari mjini Brussels kuwa ni jambo lisilokuwa la haki kuendelea kuweka vikwazo hivyo dhidi ya China , miaka 16 baada ya kutokea tukio lililosababisha kuwekwa kwake.

Ameongeza kuwa viongozi wa jumuiya ya Ulaya wanaliangalia sana hivi sasa suala la haki za binadamu.

Jana rais wa Ufaransa Jacques Chirac alijaribu kuondoa wasi wasi juu ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo na umoja wa Ulaya , akisema kuwa hakuna maana kuwa mataifa hayo yataanza kuuza silaha kwa China mara moja.