1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Sheria moja kuhusu wakimbizi

2 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfB

Halmshauri ya Umoja wa Ulaya imependekeza kuwa na sheria zinazofanana kuhusika na suala vipi nchi za Umoja huo zitawarejesha nyumbani watu walioshindwa kufanikiwa katika maombi yao ya ukimbizi na pia kuhusu wahamiaji walioingia kinyume na sheria.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Halmashauri kukiri kwamba ni theluthi moja tu ya wale waliofukuzwa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya waliondoka.Waziri wa sheria wa Umoja huo,Franco Frattini amependekeza kipindi cha miezi sita cha kuwaweka ndani wale wanaongojea kurejeshwa makwao.Vile vile amependekeza kuwa mtu anaepigwa marufuku katika nchi moja ataweza kukataliwa kuingia nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya kwa muda wa miaka mitano.Kwa hivi sasa nchi za Umoja wa Ulaya zina sheria tofauti kuhusu utaratibu wa kuwaweka ndani na kuwafukuza watu walioshindwa kupata ukimbizi.Kwa upande mwingine, makundi yanayotetea haki za binadamu yamesema yana khofu kuhusika na hatua ya kuwarejesha kwa nguvu wahamiaji katika nchi ambako kuna wasi wasi kuhusu haki za binadamu.