1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mazungumzo ya kuiingiza Uturuki katika umoja wa Ulaya huenda yataanza kesho Jumatatu.

2 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVc

Mkuu wa idara ya sera za kigeni katika umoja wa Ulaya , Javier Solana , anaimani kuwa makubaliano yanaweza kufikiwa kabla ya mazungumzo yanayopangwa kulenga kuiingiza Uturuki katika umoja wa Ulaya hapo Jumatatu.

Katika mahojiano na gazeti moja la Ujerumani, Bild am Sonntag, Solana amesisitiza , hata hivyo kuwa , mazungumzo hayo pekee hayaipi Uturuki uhakika wa kukubaliwa kujiunga na kundi hilo la mataifa.

Austria inasisitiza kuwa Uturuki ipewe kile kinachojulikana kama mshirika mpendelewa, katika umoja huo.

Katika mazungumzo ya simu na kansela wa Austria Wolfgang Schüssel jana Jumamosi , waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amerudia dai la Uturuki kuwa ipewe uanachama kamili wa umoja huo wa Ulaya. Mawaziri 25 wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya watajaribu kuondoa tofauti zao katika mkutano wa dharura nchini Luxembourg leo Jumapili.