1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mawaziri wa umoja wa Ulaya wajadili tatizo la wahamiaji wa Afrika

13 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESQ

Mawaziri wa sheria wa umoja wa Ulaya wamekutana kujadili tatizo la wahamiaji wa kiafrika wanaojaribu kuingia Ulaya kupitia Theuta na Meliya katika pwani ya kazkazini ya Moroko. Waafrika 11 wamefairiki dunia katika majuma machahe yaliyopita walipokuwa wakijaribu kuvuka sing´eng´e kwenye eneo hilo.

Moroko kwa upande wake imelaumiwa kwa kuwarudisha makwao mamia ya wahamiaji, wengi wao kutoka Senegal. Jumatatu iliyopita raia 280 wa Senegal walirudishwa nchini humo kutoka Moroko.