1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mahmud Abbas akutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya

2 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaD

Siku moja baada ya kushiriki kwenye mkutano wa kimataifa juu ya mashariki ya kati mjini London, kiongozi wa wapalestina MAHMUD ABBAS, hii leo amekuwa na mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya.

Mada muhimu kwenye mazungumzo yao ilikuwa ni misaada ya maendeleo kwa Wapalestina.

Kwenye mkutano wa jana, jumuiya ya kimataifa iliahidi kuwasaidia wapalestina kwenye ujenzi wa taifa lao.

Waisrael na Wapalestina wametakiwa pia kutekeleza wajibu wao, kwa kulingana na mpango wa amani wa pande nne - Road Map.

Rais wa wapalestina MAHMUD ABBAS ameahidi kuboresha hali ya usalama kwenye maeneo ya utawala wa ndani.

Waziri mkuu wa Uingereza, TONY BLAIR, aliyeitisha mkutano huu amesema, mkutano huu ni hatua muhimu ya kupatikana kwa suluhu ya haki, kati ya Waisrael na Wapalestina. Hata hivyo kiongozi huyu alishindwa kuwakutanisha mahasimu wote wawili kwenye mkutano huo.