1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels: Kamisheni kuu ya Umoja wa ulaya imekosoa vikali uamuzi wa ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFt1
Marekani wa kuzitenga na ujenzi mpya wa Iraq nchi zilizokataa kuunga mkono vita nchini humo.Kamisheni kuu ya umoja wa Ulaya imeutaja kua ni kosa uamuzi wa Marekani.Msemaji wa kamisheni kuu amezungumzia uwezekano wa kutumwa mashtaka mbele ya shirika la biashara la kimataifa.Wizara ya ulinzi ya Marekani imejitetea na kusema uamuzi huo haujalengwa kuwaadhibu wapinzani wa vita vya Iraq.Msemaji wa pentagon amesema hatua hiyo ni nasaha kwa serikali husika ziamue kutuma wanajeshi wao nchini Iraq.Kabla ya hapo rais George W. Bush alikua na mazungumzo pamoja na kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani,rais Jacques Chirac wa Ufaransa na mwenzake wa Rashia Vladimir Putin.